Fund ya Fidia

Exness ni mwanachama wa Tume ya Fedha, shirika la kimataifa linalojishughulisha na utatuzi wa mizozo katika tasnia ya huduma za kifedha kwa soko la forex.

Tume ya Fedha ilianzishwa ili iwe kamati ya washirika wengine isiyoegemea upande wowote ili kukagua na kutatua malalamiko kwa haki. Inalenga kuwezesha utatuzi rahisi na wa haraka kuliko kupitia wasimamizi wa sekta na mfumo wa kisheria.

Tume hii huhakikisha kwamba wafanyabiashara na mizozo ya brokers inatatuliwa kwa haraka, kwa ufaafu, bila upendeleo na kwa uhalisia, huku ikihakikisha kwamba pande zote zinapata jibu la haki na la kina kwa masuala yao. Tume hii pia hutoa ulinzi wa ziada kwa wafanyabiashara kwa kutumia Fund ya Fidia.

Imebainika kuwa Tume ya Fedha ni shirika huru la utatuzi wa mzozo wa nje (EDR).

Je, inafuata utaratibu upi?

Fund ya Fidia hutumika kama sera ya bima kwa wateja wa wanachama. Fedha hii huhifadhiwa katika akaunti tofauti ya benki na hutumiwa tu mwanachama anapokataa kuzingatia uamuzi wa Tume ya Fedha.

Je, Fund ya Fidia hulipwa vipi?

Fund ya Fidia hulipwa na Tume ya Fedha kupitia mgao wa 10% ya ada za kila mwezi za uanachama.

Je, ni nani anayelindwa?

Fund hiyo itatumika tu kwa uamuzi ambao umetolewa na Tume ya Fedha. Hazina hailindi dhidi ya hasara ya wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara inayojitegemea. Pia haitumiki kwa msingi mzima wa mteja wa wakala iwapo broker atakuwa mfilisi.

Je, ni kiwango gani cha juu cha kulindwa?

Hazina ya Fidia itashughulikia tu hukumu zinazotolewa na Tume ya Fedha ya hadi €20,000 kwa kila mteja.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali rejelea tovuti ya Tume ya Fedha na Mkataba wetu wa Mteja.

Boresha jinsi unafanya biashara

Jionee mwenyewe kwa nini Exness ndiye broker anayefaa zaidi kwa traders zaidi ya 700,000 na washirika 64,000.