Kuweka na Kutoa pesa
Chagua kutoka kwa chaguo rahisi za malipo katika sarafu za nchi yako, ikiwa ni pamoja na mifumo ya malipo maarufu zaidi duniani, pochi za kielektroniki.
Kuweka pesaKiasi cha chini zaidi cha pesa | Kasi | Kutoa pesaKiasi cha chini zaidi cha pesa | Kasi |
---|
Sheria za jumla za kuweka na kutoa pesa
Je, kuweka na kutoa pesa papo hapo kunafanyika kwa kasi gani?
Neno "papo hapo" linaonyesha kuwa transaction itafanywa ndani ya sekunde chache bila uchakataji wenyewe na wataalamu wetu wa idara ya fedha. Tafadhali kumbuka kuwa ingawa inachakatwa papo hapo kwa upande wetu, ombi lako la kuweka au kutoa fedha linaweza kuchukua muda kushughulikiwa kwa upande wa mtoa huduma wa mfumo wa malipo.
Je, inachukua muda gani kutoa fedha kupitia kadi ya benki?
Kwa upande wa Exness maombi yote ya utoaji fedha hushughulikiwa papo hapo. Kisha ombi hilo hutumwa kwa vichakataji kadi vyetu na kwa benki yako, na mchakato mzima unaweza kuchukua kutoka siku 7 hadi 10 za kazi ili funds zionekane katika akaunti yako ya benki.
Je, ninaweza kutoa funds kwa akaunti ambayo si yangu?
Fedha zinaweza kutolewa kwa akaunti zako za kibinafsi pekee. Hii ni hatua ya ulinzi uliowekwa ili kuhakikisha usalama wa kifedha.
Je, kuna ada au kamisheni yoyote?
Ingawa Exness haitozi ada, mtoa huduma wa kadi yako ya mkopo, benki au mfumo wa malipo unaweza kukutoza ada ya transaction au ada ambayo iko nje ya udhibiti wetu.
Je, ninaweza kutumia akaunti gani kuweka na kutoa pesa?
Lazima utumie akaunti yako ya malipo ya kibinafsi kwa uwekaji na utoaji pesa. Hatutaruhusu malipo ya moja kwa moja au malipo kwa wahusika wengine. Taarifa zote unazozihitaji kuhusu transactions zinaweza kupatikana katika Eneo lako la Binafsi.
Je, ni lini ninaweza kuweka na kutoa pesa?
Uwekaji na utoaji pesa unaweza kutekelezwa 24/7. Ikiwa uwekaji au utoaji pesa si wa papo hapo, tutauchakata ndani ya saa 24. Kumbuka, inaweza kuchukua benki yako au huduma ya malipo kwa muda mrefu zaidi.
Hatuwezi kuwajibikia ucheleweshaji wowote wa uchakataji wa uwekaji au utoaji pesa unaosababishwa na mifumo ya malipo.
Je, ninawezaje kutoa pesa ikiwa ninatumia mifumo mingi ya malipo?
Ukifadhili akaunti yako ya biashara kwa kutumia mifumo mingi ya malipo au pochi nyingi ndani ya mfumo sawa wa malipo, lazima funds zitolewe kulingana na kiasi kilichowekwa.
Je, muda wa uchakataji unaweza kubadilika?
Tuna haki ya kubadilisha muda wa uchakataji wa uwekaji au utoaji pesa bila kutoa arifa ya awali.
Je, njia zote za malipo zinapatikana kimataifa?
Tunaweza kuweka vikomo kwa mifumo ya malipo inayopatikana kwa wateja kutoka nchi fulani.
Je, ninaweza kutoa pesa bila kufanya biashara?
Tuna haki ya kuchunguza, kughairi, na/au kutoza ada/malipo (inategemea njia ya malipo) kwa ombi lolote la kutoa pesa linalotoka kwa akaunti ya biashara isiyo na shughuli za biashara. Kwani, madhumuni ya uwekaji na utoaji pesa ni kufadhili shughuli yako ya biashara.
Weka pesa sasa
Inachukua dakika 3 pekee kuweka mipangilio ya akaunti yako na kuwa tayari kufanya biashara